• Login
    View Item 
    •   Repository Home
    • Research Journal Articles
    • Department of Education
    • View Item
    •   Repository Home
    • Research Journal Articles
    • Department of Education
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Uhusika katika Fasihi Bulibuli ya Kiswahili: Mfano Kutoka Utenzi wa Mikidadi na Mayasa

    Thumbnail
    View/Open
    Uhusika_katika_Fasihi_Bulibuli_ya_Kiswahili_Mfano_.pdf (254.7Kb)
    Date
    2024
    Author
    Burundi, Rosemary N
    Mugambi, Allan
    M’Ngaruthi, Timothy K
    Metadata
    Show full item record
    Abstract
    Makala hii inatathmini uhusika wa wahusika katika tenzi za Kiswahii kwa kuegemea utenzi mmoja bulibuli: Utenzi wa Mikidadi na Mayasa. Utenzi huu ulitungwa na Saidi Abdallah Masudi el Buhry aliyekuwa mkazi wa Pemba. Ingawa Masudi aliishi Pemba kwa muda, alihamishwa kwenda Mtang’ata, kilomita kumi kusini mwa Tanga alipohudumu kama gavana wa utawala wa Kimazrui. Bwana Masud alikuwa mshairi mtajika kwa tungo zake nyingi. Utenzi huu ni mmojawapo wa kazi zake zilizotia fora katika janibu ya Waswahili wakati huo. Allen (1971) anasema kuwa utenzi wa Mikidadi na Mayasa unahusu mashujaa wa wakati wa mtume Mohammed (SAW) na baada ya kufariki kwake. Kipengele cha wahusika ni muhimu katika kutunga kazi yoyote ya kifasihi. Kinashirikishwa na vipengele vingine vya kifani ili kuwezesha mtunzi kutoa maudhui au ujumbe wake. Watunzi wa kazi ya kifasihi huwajenga wahusika kisanaa ili waweze kuwakilisha vipengele vingi katika maisha ya jamii wanayotungia. Watunzi pia hutumia mbinu mbalimbali kuwasawri wahusika kutegemea tajriba yao ya kisanii pamoja na utanzu unaoshughulikiwa. Makala hii inafafanua baadhi ya mbinu zilizotumiwa na mtunzi kuwajenga wahusika wa aina mbalimbali waliojitokeza katika Utenzi wa Mikidadi na Mayasa. Pia inabainisha kuwa ushairi, hasa tenzi huwa na wahusika waliojengwa kikamilifu kwa kutumia mbinu mbalimbali za kimtindo na za lugha. Huu ni utafiti wa maktabani. Uliongozwa na nadharia ya Umitindo hasa mawazo ya Leech (1969). Alisisitiza umuhimu wa lugha kama chombo tekelezi kinachosaidia mtunzi wa kazi ya fasihi kuwasilisha ujumbe wake. Uchanganuzi wa matini za kifasihi kwa kutumia Umitindo unaweza kutekelezwa kwa kuchunguza jinsi mwandishi amefinyanga lugha kisanii ili kuwasilisha ujumbe, kuchunguza msuko na sifa za kimuundo za kazi, mbinu za usimulizi na mikabala ya kimtazamo anayochukua mwandishi Aidha, Umitindo unahusisha uchunguzi wa uteuzi wa wahusika, mandhari na lugha yao, hulka na sifa zao zinazowezesha mtunzi kuwatumia kuakisi masuala fulani katika jamii anayotungia. Nadharia hii ilikuwa muhimu katika utafiti huu uliolenga kutathmini uhusika au mikakati iliyotumiwa na mtunzi kuwasawiri wahusika. Wahusika kama nyenzo kuu huteuliwa
    URI
    http://repository.tharaka.ac.ke/xmlui/handle/1/4361
    Collections
    • Department of Education [38]

    Tharaka University copyright © 2020  Repository
    Contact Us | Send Feedback
    Designed by
    TUN Library
     

    TUN
     

     

    Browse

    All of RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Tharaka University copyright © 2020  Repository
    Contact Us | Send Feedback
    Designed by
    TUN Library
     

    TUN